Je, Fasta Online hutoa huduma zipi?
Tunatoa huduma mbalimbali kama maombi ya NIDA, vyeti vya kuzaliwa, TIN number, CV guide, updates za ajira, internships, na zaidi.
Ninawezaje kuomba huduma?
Tembelea ukurasa wa huduma, chagua huduma unayotaka na bonyeza button ya "Omba Huduma". Utapelekwa kwenye fomu ya kujaza taarifa zako.
Huduma zinalipiwa?
Baadhi ya huduma ni bure (kama updates za ajira), lakini huduma maalum kama kuandaa CV, maombi ya cheti au leseni zinahitaji malipo kidogo kulingana na aina ya huduma.
Je, nitalipaje huduma?
Tunapokea malipo kwa njia ya simu (M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money). Maelezo ya malipo yatatumwa mara baada ya kujaza fomu yako.
Huduma zenu zinapatikana nchi nzima?
Ndio! Huduma zetu zinatolewa mtandaoni hivyo mteja yeyote ndani au nje ya Tanzania anaweza kuwasiliana nasi na kupata huduma.
Naweza kuangalia matokeo ya NECTA kupitia Fasta Online?
Ndio! Tunakuwezesha kuangalia matokeo ya:
- Kidato cha Nne (CSEE)
- Kidato cha Sita (ACSEE)
- Darasa la Saba (PSLE)
- Matokeo ya QT na Mock
Unaweza kutumia namba yako ya mtihani na mwaka husika kupata matokeo yako moja kwa moja.
Ninawezaje kuhakiki udahili wangu wa chuo?
Tunatoa huduma ya kuhakiki udahili kwa:
- Vyuo Vikuu vyote Tanzania (kupitia TCU)
- Vyuo vya Kati na VETA
- Uhakiki wa malipo ya ada
- Ushauri wa kozi na vyuo
Weka namba yako ya TCU au namba ya udahili kuangalia status yako.
Kuna msaada wa ziada kwa wanafunzi?
Tunawapa wanafunzi:
- Past papers na majibu
- Maktaba ya online ya vitabu
- Kozi za online
- Ushauri wa kitaaluma
- Fursa za masomo na scholarship
Je, naweza kupata msaada wa maombi ya vyuo?
Ndio, tunasaidia katika:
- Kujaza fomu za maombi ya vyuo
- Kuandaa nyaraka zinazohitajika
- Kufuatilia maombi yako
- Ushauri wa kuchagua programu sahihi
Muda wa kupata huduma ni upi?
Muda hutofautiana kulingana na huduma:
- Matokeo ya mitihani - Mara moja
- Uhakiki wa udahili - Dakika 30
- Ushauri wa kitaaluma - Siku 1-2
- Maombi ya vyuo - Siku 2-3
Kwa huduma za haraka, wasiliana nasi moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Gharama za huduma ni zipi?
Bei zetu ni nafuu na zinategemeana na huduma:
- Matokeo ya mitihani - Bure
- Uhakiki wa udahili - TSh 2,000
- Ushauri wa kina - TSh 5,000
- Msaada wa maombi - TSh 10,000
Malipo yote yanafanyika kupitia simu: M-Pesa, Tigo Pesa, na Airtel Money.