TRA Services

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Huduma Bora za Kodi na Ushuru Kupitia Fasta Online

Kuhusu TRA

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ni taasisi ya serikali inayosimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani na ya forodha kwa ajili ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. TRA ina jukumu la kuhakikisha kodi na tozo mbalimbali zinakusanywa kwa ufanisi, kwa uwazi, na kwa mujibu wa sheria.

Huduma Zinazotolewa na TRA

Usajili wa TIN

Usajili wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kwa watu binafsi na kampuni

Fasta Online: Jinsi Tunavyoweza Kukusaidia kwa Huduma za TRA

Kupitia Fasta Online, tunaleta karibu kwako huduma za TRA kwa njia rahisi, ya haraka, na isiyo na usumbufu. Hatuhusiani moja kwa moja na TRA, lakini tunasaidia watu kwa njia ya usaidizi wa kiteknolojia na huduma za kiwakala.

Huduma Tunazotoa Kuhusu TRA

Usaidizi wa kuomba TIN number (binafsi au ya kampuni)

Usaidizi wa kujaza fomu za kodi na kuwasilisha online

Maombi ya leseni za biashara kupitia mfumo wa BRELA na TRA

Kusaidia kuanzisha akaunti ya mtandaoni ya TRA (portal)

Ushauri kwa watu wanaotaka kuanza biashara kuhusu kodi

Kusaidia kutuma barua au maombi maalum kwa TRA kwa njia rasmi

Faida za kutumia Fasta Online

Hakuna foleni wala usumbufu

Msaada wa moja kwa moja kwa njia ya simu, WhatsApp au tovuti

Tunafuatilia mpaka huduma yako ikamilike

Ushauri wa kitaalamu na uaminifu

Mawasiliano ya TRA

Benjamin Mkapa Tower, Samora Avenue

S.L.P. 11491, Dar es Salaam, Tanzania

+255 22 211 9591

www.tra.go.tz