NIDA Services

Huduma Bora za Utambulisho wa Taifa

NIDA

Kuhusu NIDA

NIDA (National Identification Authority) ni taasisi ya serikali ya Tanzania iliyoanzishwa rasmi mwaka 2008 kwa lengo la kusimamia usajili na utambuzi wa watu nchini. Majukumu yake ni pamoja na:

Huduma Zinazotolewa na NIDA

Usajili wa Raia na Wageni Wakaazi

Kwa njia ya mtandao kupitia eonline.nida.go.tz au kwa njia ya kawaida katika ofisi za NIDA.

Usajili wa Watanzania waishio Nje ya Nchi

Huduma hii ilianza kwa Watanzania waishio Marekani na inaendelea kupanuliwa kwa nchi nyingine.

Marekebisho ya Taarifa

Kama majina, tarehe ya kuzaliwa, au taarifa nyinginezo.

Kuhuisha au Kubadilisha Kitambulisho

Kwa waliopoteza au kuharibikiwa na kitambulisho.

Huduma kwa Wadau

Kama taasisi za kifedha, waajiri, na mashirika mengine yanayohitaji kuhakiki taarifa za wateja wao.

Huduma Mtandao (Self Service)

Kupata Namba ya Utambulisho wa Taifa (NIN), kufuatilia hali ya maombi, kujisajili kimtandao, kuhakiki taarifa, na kupata namba ya malipo ya serikali.

Tovuti Rasmi na Huduma Mtandao

Ofisi za NIDA

NIDA ina ofisi katika wilaya zote za Tanzania Bara na Zanzibar. Kwa Dar es Salaam, ofisi ziko katika maeneo yafuatayo:

Kinondoni

Kawe - Karibu na viwanja vya Tanganyika Packers.

Kigamboni

Gezaulole - Jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kigamboni.

Temeke

Usalama - Karibu na kituo cha Polisi Chang'ombe.

Ilala

Ukonga - Mombasa, karibu na gereza la Ukonga.

Ubungo

Kibamba - Jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo.

Mawasiliano

Simu: +255 673 333 444 / 0800 758 888 (bure) / +255 22 266 4168

Barua pepe: info@nida.go.tz

Anuani: S.L.P 12324, Dar es Salaam, Tanzania

Tuma Ombi Lako

Unahitaji Msaada na Huduma za NIDA?

Sisi ni wakala rasmi wa kusaidia kupata huduma za NIDA kwa urahisi na haraka. Tunaweza kukusaidia katika usajili, marekebisho ya taarifa, ufuatiliaji wa maombi, na huduma nyingine zote za NIDA. Wasiliana nasi leo kwa huduma ya kitaalamu na ya kuaminika!

Wasiliana Nasi Leo