Fasta Online Logo

Nafasi za Kazi

Taarifa Muhimu: Mabadiliko ya Mfumo wa Maombi ya Kazi

Taarifa kwa Waombaji Kazi Wote

Mabadiliko yaliyofanywa kwa waombaji kazi wenye akaunti kwenye mfumo wa ajira kuanzia tarehe 6 Januari, 2020.

Kama huwezi kuona PDF, bofya hapa: Pakua PDF

Taarifa Muhimu: Usahihishaji wa Taarifa za Waombaji

Waombaji Wanatakiwa Kuhuisha Taarifa

Taarifa za Utambulisho

Waombaji wote wanatakiwa kuhuisha taarifa zao kwa:

  • Kuweka namba ya NIDA (NIN) kwenye sehemu ya "Personal Details"
  • Kuhakikisha taarifa zinafanana na kitambulisho cha NIDA
Sifa za Kitaaluma

Katika sehemu ya "Academic Qualification":

  • Weka kozi yako katika Category husika
  • Hakikisha vyeti vyote vimewekwa kwa usahihi
Kuangalia Status ya Maombi
  1. Ingia kwenye akaunti yako
  2. Nenda kwenye "MY APPLICATION"
  3. Utaona:
    • Namba ya usaili (kwa waliofanikiwa)
    • Sababu za kutokuitwa (kwa wasiofanikiwa)

Kusoma taarifa kamili: Pakua PDF

Nafasi za Kazi - Uchaguzi Mkuu 2025 Mpya

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Tanzania Nzima Muda wa Siku Nne Deadline: 10/07/2025

NEC inatangaza nafasi za kazi za muda mfupi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu 2025. Nafasi hizi ni kwa ajili ya kusimamia na kuratibu shughuli za uchaguzi...

Sifa za Mwombaji:

  • Awe Mtanzania
  • Awe na umri kuanzia miaka 18
  • Aweze kuandika na kusoma
  • Awe na uwezo wa kutumia simu au kompyuta
  • Asiwe kiongozi wa chama chochote cha siasa

Malipo ya Kila Siku:

  • Posho: TZS 40,000/=
  • Chakula: TZS 10,000/=
  • Nauli: TZS 10,000/=

Jumla kwa Siku: TZS 60,000/=

Muda wa Kazi:

  • Siku nne (4) za kazi
  • Mafunzo yatatolewa kabla ya kuanza kazi

Muhimu:

  • Nafasi ni za muda mfupi (temporary)
  • Waliochaguliwa watatakiwa kuwa tayari kufanya kazi katika maeneo watakayopangiwa
  • Maombi yafike kabla ya tarehe 10/07/2025

MATOKEO YA USAILI AJIRA PORTAL Mpya

Ajira Portal Tanzania Deadline: 07/05/2025

Matokeo ya usaili wa kujiunga na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania uliofanyika tarehe 07/05/2025...

Maelezo:

  • Matokeo ya usaili wa kujiunga na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
  • Usaili ulifanyika tarehe 07/05/2025
  • orodha ya majina ya waliochaguliwa

Majina ya Mafunzo - Jeshi la Zimamoto 2025 Mpya

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Chogo - Handeni, Tanga Waliochaguliwa kwa Mafunzo Kuripoti: 16/05/2025 - 18/05/2025

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linatangaza majina ya waliochaguliwa kuhudhuria mafunzo ya Uaskari ngazi ya Konstebo...

MHASIBU DARAJA LA II (ACCOUNTANT II) Mpya

MDAs & LGAs Nafasi: 20 Deadline: 11/05/2025

Nafasi za Uhasibu katika Taasisi za Serikali na Serikali za Mitaa.

Majukumu ya Kazi:

  • Kuandika taarifa ya mapato na matumizi
  • Kuandika taarifa za maduhuli
  • Kupokea maduhuli ya serikali na kupeleka Benki kwa wakati
  • Kufanya usuluhisho wa hesabu za Benki
  • Kukagua hati za malipo
  • Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa

Sifa Zinazohitajika:

  • Shahada ya Uhasibu/Biashara AU Stashahada ya juu ya Uhasibu
  • Cheti cha CPA(T) au sifa inayolingana kutoka NBAA
  • Kuwa na Kidato cha Sita

Mshahara:

TGS.E kwa mujibu wa ngazi za mishahara serikalini

Assistant Lecturer - Urban Planning Mpya

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) Mbeya Nafasi: 1 Deadline: 08/05/2025

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kinatangaza nafasi ya kazi ya Assistant Lecturer katika fani ya Urban Planning/Urban and Regional Planning...

Majukumu ya Kazi:

  • Kufundisha na kuendesha semina kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza
  • Kuandaa na kuwasilisha case studies
  • Kufanya na kuchapisha matokeo ya utafiti
  • Kutambua na kusaidia wanafunzi wenye changamoto za masomo
  • Kushiriki katika ushauri na huduma za jamii chini ya usimamizi
  • Kuhudhuria warsha na mikutano ya kitaaluma

Sifa za Mwombaji:

  • Shahada ya Uzamili katika mojawapo ya fani zifuatazo:
    • Urban Planning and Management
    • Urban and Regional Planning
    • Geographical Information Systems
    • Infrastructure Development and Management
    • Transport Planning
    • Urban Design
  • GPA ya 4.0/5.0 katika Shahada ya Uzamili
  • Shahada ya kwanza katika fani husika na GPA ya 3.8/5.0
  • Alama ya B+ au zaidi katika tasnifu

Mshahara:

PUTS 2.1

Senior Training Officer Mpya

Platinum Credit LTD Dar es Salaam Full Time Deadline: 31/12/2023

Platinum Credit Limited ni kampuni ya mikopo midogo midogo iliyosajiliwa Tanzania chini ya Sheria ya Makampuni...

Majukumu ya Kazi:

  • Kutambua na kufuatilia mahitaji ya mafunzo katika kampuni
  • Kubuni, kupanga na kutekeleza mipango ya mafunzo, sera na taratibu
  • Kuhakikisha ukuaji na ubaki wa wawakilishi wa mauzo
  • Kuimarisha kuridhika kwa wateja kupitia mipango madhubuti ya mafunzo

Sifa za Mwombaji:

  • Shahada ya kwanza katika fani ya biashara, elimu au Usimamizi wa Rasilimali Watu
  • Uzoefu wa angalau miaka miwili
  • Ujuzi wa Usimamizi wa Miradi
  • Uwezo wa Uongozi na Mahusiano ya Kijamii
  • Uwezo wa Uchambuzi na Utatuzi wa Matatizo
  • Ujuzi wa Uwezeshaji na Ufundishaji
  • Ujuzi wa Mawasiliano na Uwasilishaji

Jinsi ya Kuomba:

  • Tuma CV na barua ya maombi pamoja na vyeti vyote vya elimu
  • Tuma kupitia barua pepe: careers@platinumcredit.co.tz
  • Andika: "SENIOR TRAINING OFFICER" kwenye sehemu ya subject

Operation and Administration Executive Mpya

Fracama Company Ltd Kibaha - Pwani Full Time Deadline: 16/05/2025

Msimamizi wa Uendeshaji na Utawala atakuwa na jukumu la kusimamia nyanja zote za uendeshaji wa kampuni zinazohusiana na kitengo cha vifaa vya ujenzi...

Maelezo ya Kazi:

Nafasi hii inahitaji mtu mwenye uwezo wa kufikiria kimkakati, ujuzi wa uongozi na uelewa wa kina wa sekta ya ujenzi. Atawajibika kuongeza mapato, kuhakikisha ufanisi wa utendaji, na kudumisha viwango vya juu vya kuridhisha wateja.

Majukumu Makuu:

  • Kupanga Mikakati: Kuunda na kutekeleza mipango ya kimkakati
  • Usimamizi wa Fedha: Kusimamia utendaji wa kifedha, bajeti na udhibiti wa gharama
  • Mauzo na Masoko: Kuongoza ukuaji wa mauzo kupitia mikakati bora
  • Usimamizi wa Operesheni: Kuhakikisha uendeshaji fanisi
  • Uongozi wa Timu: Kuongoza na kuendeleza timu yenye utendaji wa hali ya juu
  • Uzingatiaji: Kuhakikisha uzingatiaji wa kanuni zote husika
  • Huduma kwa Wateja: Kudumisha viwango vya juu vya kuridhisha wateja
  • Uchambuzi wa Soko: Kufuatilia mienendo ya soko
  • Kujenga Mahusiano: Kujenga mahusiano imara na wadau muhimu

Sifa Zinazohitajika:

  • Shahada ya kwanza katika fani ya Biashara, Uhasibu, Utawala au fani inayohusiana
  • Uzoefu wa miaka 2+ katika nafasi ya uongozi
  • Uzoefu katika sekta ya vifaa vya ujenzi ni faida ya ziada
  • Ujuzi mzuri wa kifedha na uwezo wa kupanga bajeti
  • Uwezo bora wa uongozi na usimamizi wa timu

Jinsi ya Kuomba:

  • Tuma maombi yako kupitia:
  • Barua pepe: fracama.hr@gmail.com
  • Sanduku la Posta: P.O. Box 30203, Kibaha - Pwani

Reliability Superintendent Mpya

Barrick Africa Middle East Tanzania Full Time Deadline: 31/05/2025

The Barrick Africa Middle East Team is seeking to recruit a Reliability Superintendent to join and grow our team...

Barrick's Core Values:

  • Communicating Honestly, Transparently, and Acting with Integrity
  • Exhibiting a Results-Driven approach
  • Delivering solutions that are Fit for Purpose
  • Dedicating to Building a Sustainable Legacy
  • Taking Responsibility and being Accountable
  • Committing to Zero Harm
  • Cultivating strong and meaningful Partnerships

Key Responsibilities:

  • Managing safe working behaviors of the reliability team
  • Analyzing plans and developing reliability-engineering programs
  • Leading engineering root cause analysis
  • Managing KPIs including MTBF and MTTR
  • Implementing Quality Assurance on critical equipment
  • Asset Management Framework implementation
  • Warranty Management and CBM team supervision

Health and Safety Responsibilities:

  • Ensuring DUTY of CARE responsibilities
  • Implementing critical controls for Fatal Risk tasks
  • Maintaining Zero incident/accident policy
  • Conducting regular Safety Interactions

Qualification Requirements:

  • Bachelor's degree in Mechanical Engineering or equivalent
  • Professional Engineering Certification
  • 5+ years Maintenance Engineer experience in Mining Industry
  • 2+ years maintenance budget management experience
  • Strong computer skills including SAP
  • Previous experience in Africa preferred

Benefits:

  • Comprehensive compensation package with bonuses
  • Career growth opportunities
  • Dynamic and collaborative work environment
  • Site-specific benefits

Assistant Technician (Mineral Laboratory) - 6 Posts Mpya

Geological Survey of Tanzania (GST) Tanzania Nafasi 6 Deadline: 14/05/2025
Omba Kazi

Ajira Mpya - Jeshi la Polisi Tanzania Mpya

Jeshi la Polisi Tanzania Tanzania Nzima Form IV, VI, Diploma & Degree Deadline: 04/04/2025

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania anatangaza nafasi za ajira kwa vijana wa kitanzania wenye elimu ya Shahada, Stashahada, Astashahada, Kidato cha sita na Kidato cha nne...

Sifa za Msingi za Muombaji:

  • Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa
  • Wazazi wake wawe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa
  • Umri: miaka 18-25 (Form IV/VI & Diploma), 18-30 (Degree)
  • Urefu: Wanaume futi 5'8", Wanawake futi 5'4"
  • Awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto
  • Awe na afya njema kimwili na kiakili

Elimu na Sifa za Kitaaluma:

  • Kidato cha IV: Division I-IV (Points 26-28 kwa Division IV)
  • Kidato cha VI: Division I-III
  • Wahitimu wa miaka 2019-2024
  • Shahada (NTA 8), Stashahada (NTA 6), Astashahada (NTA 5/NVA 3)

Mahitaji Muhimu:

  • Kitambulisho cha Taifa au namba ya NIDA
  • Uwezo wa kuongea Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha
  • Asiwe na alama za kuchorwa mwilini (tattoo)
  • Asiwe na kumbukumbu za uhalifu
  • Awe tayari kufanya kazi mahali popote Tanzania

Jinsi ya Kuomba:

  • Andika barua ya maombi kwa mkono (handwriting)
  • Tuma maombi kupitia: https://ajira.tpf.go.tz
  • Ambatisha barua ya maombi kwenye mfumo kama PDF
  • Jigharamie katika hatua zote za usaili

Nafasi za Kuandikishwa Jeshini - JWTZ Mpya

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Tanzania Form IV - PhD Deadline: 14/05/2025

JWTZ linatangaza nafasi za kuandikishwa Jeshini kwa vijana wa Kitanzania wenye elimu kuanzia elimu ya Sekondari hadi elimu ya Juu, pamoja na wenye Taaluma Adimu...

Sifa za Mwombaji:

  • Awe raia wa Tanzania mwenye kitambulisho cha Taifa
  • Awe na afya nzuri na akili timamu
  • Mwenye tabia na nidhamu nzuri
  • Awe na cheti halisi cha kuzaliwa na vyeti vyote vya elimu
  • Awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza au Kikosi cha Kuzuia Magendo
  • Awe amehitimu mafunzo ya JKT

Umri:

  • Kidato cha 4 & 6: Usiozidi miaka 24
  • Stashahada: Usiozidi miaka 26
  • Shahada: Usiozidi miaka 27
  • Madaktari Bingwa: Usiozidi miaka 35

Taaluma Adimu Zinazohitajika:

  • Madaktari Bingwa (Surgeons, Specialists)
  • Medical & Dental Doctors
  • Wahandisi (Electronic, Mechanical, Marine)
  • Aviation & Aeronautical Specialists
  • Mafundi Welding & Metal Fabrication

Jinsi ya Kuomba:

  • Andika barua ya maombi kwa mkono
  • Ambatisha nakala za vyeti vyote vinavyohitajika
  • Ambatisha nakala ya kitambulisho cha Taifa/NIDA
  • Ambatisha namba ya simu ya mkononi